02 Jun 2026
- 02 Jun 2026
09:00
- 18:00
ASTEVALOCY (MACHEYEKI HALL)
Youth Agribusiness and Skills Forum ni jukwaa maalum linalolenga kuwawezesha vijana kwa kuwajengea uelewa, ujuzi na mtazamo chanya kuhusu fursa zilizopo katika sekta ya kilimo ,ujasiriamali na uongozi
Semina hii inalenga kuhamasisha vijana kuona kilimo kama ajira yenye tija na fursa ya kujiajiri, badala ya kukiona kama shughuli ya kawaida isiyo na thamani. Kupitia mjadala na mafunzo ya vitendo, washiriki watapata maarifa kuhusu namna ya kuanzisha na kuendesha miradi ya kilimo kibiashara (agribusiness), pamoja na mbinu bora za kuongeza thamani ya mazao.
Aidha, semina itatoa ujuzi muhimu (skills) zinazohitajika katika soko la ajira na biashara, ikiwemo:
Ujasiriamali na ubunifu
Usimamizi wa fedha
Masoko na mnyororo wa thamani (value chain)
Fursa za ufadhili na mitaji kwa vijana
safari ya uongozi kwa viajana
Kupitia jukwaa hili, vijana watapata nafasi ya kujifunza, kubadilishana uzoefu, na kujenga mtandao (networking) utakao wawezesha kukua kiuchumi na kijamii.
Kwa ujumla, Youth Agribusiness and Skills Forum inalenga kuwa chachu ya mabadiliko kwa vijana kwa kuwasaidia kujitegemea, kupunguza ukosefu wa ajira, na kuchangia maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla